Loading Bible Translation
First-time download in progress. This may take a few seconds…
Swahili Bible Wordproject Bible
6 verses
1Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la uweza wake.
2Msifuni kwa matendo yake makuu; Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.
3Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi;
4Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi;
5Msifuni kwa matoazi yaliayo; Msifuni kwa matoazi yavumayo sana.
6Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana. Haleluya.