Loading Bible Translation
First-time download in progress. This may take a few seconds…
Swahili Bible Wordproject Bible
12 verses
1Mbona mataifa wanafanya ghasia, Na makabila wanatafakari ubatili?
2Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya Bwana, Na juu ya masihi wake.
3Na tuvipasue vifungo vyao, Na kuzitupia mbali nasi kamba zao.
4Yeye aketiye mbinguni anacheka, Bwana anawafanyia dhihaka.
5Ndipo atakaposema nao kwa hasira yake, Na kuwafadhaisha kwa ghadhabu yake.
6Nami nimemweka mfalme wangu Juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.
7Nitaihubiri amri; Bwana aliniambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa.
8Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako, Na miisho ya dunia kuwa milki yako.
9Utawaponda kwa fimbo ya chuma, Na kuwavunja kama chombo cha mfinyanzi.
10Na sasa, enyi wafalme, fanyeni akili, Enyi waamuzi wa dunia, mwadibiwe.
11Mtumikieni Bwana kwa kicho, Shangilieni kwa kutetemeka.
12Shikeni yaliyo bora asije akafanya hasira, Nanyi mkapotea njiani, Kwa kuwa hasira yake itawaka upesi, Heri wote wanaomkimbilia.